20 Percent azungumza kwa uchungu kuhusu BongoFleva

Msanii 20 Percent amefunguka kusema anaionea huruma jamii ya muziki wa BongoFleva kaw sababu kile ambacho kinawadhuru jamii kimetawala kwenye muziki wa sasa, pia wamekosa kutoa kitu chenye elimu.


"Tunauangalia sawa muziki wa BongoFleva japo kuna kila mtu anaufahamu wake na wakati wake katika suala hilo lakini tunautazama kwa jicho la huruma, upole, hasira na kuufurahia wakati wa furaha" amesema 20 Percent 


Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Jamii ya sasa ya wana BongoFleva naionea huruma, kwa sababu kile ambacho kinawadhuru jamii kimetawala kwenye game yetu, ni kama wakulima wasiovuna kitu kizuri karibia miaka minne au mitano sasa" 

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE