11/17/2020

Afisa LATRA aliemtishia dereva lori panga asimamishwa kaziMamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini LATRA imemsimamisha kazi Afisa wake kutoka Mkoa wa Lindi ambaye video yake imesambaa mtandaoni akimshikia silaha aina ya panga dereva wa lori lenye namba ya usajili T412 DNN kilichotokea tarehe 11/11/2020.


Mkurugenzi Mkuu wa LATRA Gilliard Ngewe amesema sasa kinachoendelea ni uchunguzi wa tukio hilo na adhabu kali zitachukuliwa kwa muhusika ndani ya siku 21 za uchunguzi kulingana na sheria za utumishi wa umma.


“Hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria dhidi ya Afisa huyo zinaendelea kuchukuliwa na hatua ya kumsimamisha kazi imechukuliwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003 ya utumishi wa umma” Mkurugenzi Mkuu LATRA

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger