Aida Khenan Amtaka Mbowe Kubadili MsimamoMbunge Mteule wa Nkasi kwa tiketi ya CHADEMA Aida Khenan amewaomba viongozi wake waangalie upya msimamo wa kutotambua ushindi wa Wabunge na Madiwani kutokana na hitilafu za Uchaguzi Mkuu.


Aida ameshikilia msimamo wake wa kuwasikiliza na kuwasimamia wananchi hivyo hawezi kukubali kuacha Ubunge ili kujiunga na wenzie katika madai yao.


Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Tanzania hakuna Mbunge binafsi, Mbunge ni wa Chama hivyo ni lazima afuate misimamo ya Chama na kusisitiza kuwa watachukua hatua zaidi wakikaa kikao cha viongozi.


Aida pia alionekana kwenye sherehe za kumuapisha Rais John Magufuli, kwenye  Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE