Ajali yamfanya Belle 9 kuimba Injili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

 
Mkali wa muziki wa RnB Belle 9 amesema ameamua kuimba wimbo wenye mahadhi ya Injili baada ya kujitafakari ndani ya nafsi yake kufuatia tukio la kupata ajali ya gari siku ya Septemba 7, akiwa na wasanii wengine ambao ni Bonge la Nyau na Lulu Diva.

 

Belle 9 amesema eneo hilo ambalo amepata ajali ni ngumu sana watu kusalimika ila yeye amefanikiwa kutoka salama ndiyo maana akaimba wimbo huo wa injili ili kumshukuru Mungu.


"Baada ya kupata ajali nilitumia muda mwingi kujitafakari ndani ya nafsi yangu, niliambiwa  eneo nililopata ajali watu wengi huwa wanapotea kabisa, kwahiyo matokeo ya kuimba ule wimbo ni baada ya kutoka salama na kutoa shukrani, nimeujua ukubwa wa mungu na sasa hivi maisha yangu yamebadilika" 


Belle 9, Bonge la Nyau na Lulu Diva walipata ajali ya gari maeneo ya Chalinze wakati wanatoka kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ilolo, Mkoani Iringa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad