Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Alichokisema Stamina kuhusu Prof Jay "Alibadili Akili za Wazee Wetu"

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


MwanaHipHop Stamina Shorwebwenzi amesema msanii na mwanasiasa Prof Jay anatakiwa heshima ya kipekee kwani amekuwa na ushawishi kwa wasanii wengine pia alibadilisha akili za wazee ambao walikuwa wanaamini muziki ni uhuni


Stamina amesema hakuna msanii wa sasa ambaye hajamsikiliza Prof Jay wakati anakuwa au akijiandaa kuingia kwenye muziki pia ameipambania 'game' ya BongoFleva mpaka kufikia hapa.


"Prof Jay ni kaka yangu au baba ana nafasi hiyo kwangu, kuna muda nikipiga naye stori namwambia simuoni kama mpinzani ila namuona kitaifa zaidi ila tunatakiwa kuheshimu maamuzi na maisha lazima yaendelee, nimefika hadi studio za Mwanalizombe Mikumi na nina ngoma naye" 


"Hakuna rapa yeyote ambaye hajawahi kumsikiliza Prof Jay, ni mmoja kati ya inspiration  kubwa kwa watu pia alibadilisha akili za wazee wetu kwamba muziki sio uhuni,kwenye maisha muogope sana mtu anayepambania watu wengine" ameongeza


Prof Jay ni mmoja kati ya wasanii wa kwanza na wenye heshima kwa kuanza muziki hapa nchini Tanzania ambapo amefanikiwa kutengeneza ngoma kali ambazo zilifanya vizuri kwenye 'chart' na kubeba tuzo mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments