"Alikiba Aliniomba Kumuandikia Mediocre" - Mkali


Mchekeshaji Mkali Wenu ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kumuandikia wimbo wa mediocre ya msanii Alikiba ambapo amesema awali wimbo huo alitaka ampatie Nay wa Mitego ila aliishindwa.


"Kitu chochote kinaweza kutokea, kama menejmenti yangu ikisema nifanye kazi na Alikiba nitafanya naye, kwa sababu Alikiba ni mshkaji wangu na namuandikia nyimbo, hata hii nyimbo aliyotoa ya mediocre nilikuwa nayo muda mrefu aliniomba nikamuandikia, ukiangalia ina utofauti na nyimbo zake zingine" amesema Mkali Wenu 


"Kumuandikia mtu haimaanishi kama hauna sauti ila Alikiba yeye ana sauti nzuri, mimi nina sauti ila sio nzuri kwenye kuimba, nyimbo ya mediocre imekaa vizuri kwake nilishawahi kumpa Nay wa Mitego akasema haiwezi kuiimba".


Aidha Mkali Wenu amesema 'role model' wake alikuwa ni marehemu Sharo Milionea ambaye alianzia kwenye uchekeshaji kisha kuimba hivyo wasishangae kumuona na yeye akianza kuimba.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments