11/11/2020

Biden Kumpendekeza Obama Kuwa Balozi wa Marekani Nchini Uingereza

 


VYOMBO vya habari vya Uingereza vimesema, kama Joe Biden akiapishwa kuwa Rais, huenda atampendekeza Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama kuwa balozi wa nchi hiyo nchini Uingereza.

Kutokana na hoja zisizo za kirafiki kuhusu rais huyo wa zamani zilizotolewa na waziri mkuu wa Uingereza Borris Johnson, uteuzi huo utaweza kuwa kikwazo kwa Boris kwa kuwa viongozi hao wawili walikuwa na mikwaruzano.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, ingawa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Marekani hayajatolewa, mgombea urais wa Chama cha Democrats Joe Biden anayeongoza katika uchaguzi huo ameanza kutekeleza mpango wa mpito, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo na kubadili sera kadhaa za serikali ya Trump

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger