Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Billboard imemtaja Rapa Cardi B kama Mwanamke Bora wa Mwaka...Nick Minaj Alie tu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Billboard imemtaja rapa Cardi B kama Mwanamke bora wa Mwaka (Woman of the Year) kwa mwaka huu. Leo Jumatano Billboard wametangaza majina ya Wanawake walio kwenye muziki ambao wamepewa tuzo za heshima kwa mwaka 2020.


Cardi B atatunukiwa tuzo hiyo ya heshima na kusheherekewa kwenye hafla ya 15 ya tuzo hizo za Wanawake waliofanya vyema kwenye tasnia ya muziki (15th Annual Women in Music Event) tukio ambalo litafanyika Disemba 10.


Wengine waliotajwa kutunukiwa tuzo hiyo ya heshima na Billboard ni mkongwe wa muziki wa Country, Dolly Parton ambaye atakabidhiwa tuzo ya (Powerhouse Award) pamoja na mwimbaji Dua Lipa. Wakali wa R&B Chloe x Halle watapokea (Rising Star Award) na wasanii wengine kibao.


Kwa mwaka huu mpaka sasa Cardi B ameachia ngoma moja tu 'WAP' aliyofanya na mkali Megan Thee Stallion, ngoma hiyo ilikaa wiki 4 katika nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard Hot 100.

Post a Comment

0 Comments