Bondia Mwakinyo Apanda Nafasi Kwenye Viwango vya Ngumi Duniani...Ashika Nafasi Hii
Bondia huyo namba moja nchini ametajwa kuwa bondia wa nyota tatu duniani, akihitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwamo #MannyPacquiao mwenye nyota tano.


Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, Boxrec saa chache zilizopita Ijumaa hii, #Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 duniani kati ya mabondia  2,050 wa uzani wa super welter.


Bondia huyo licha ya kushinda mapambano kadhaa mwaka huu likiwamo la Tshibangu Kayembe, alibaki nafasi ya 78 mpaka leo vilipotajwa viwango vipya na kupanda hadi nafasi ya 41.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments