Breaking News: Bunge Lamthibitisha Majaliwa Kwa 100% Kuwa Waziri Mkuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Bunge la Tanzania limemuidhinisha  mbunge wa Ruangwa (CCM), Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu  baada ya kupigiwa kura za ndiyo 350.

Uteuzi wa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu umefanywa na Rais John Magufuli leo Alhamisi Novemba 12, 2020 na jina lake kuwasilishwa bungeni na mpambe wa Rais.

Baada ya kuwasilishwa, Spika Job Ndugai aliwatangazia wabunge kuhusu uteuzi huo, kisha wawakilishi hao wa wananchi kupiga kura ya kumuidhinisha.

Katika ya kura 350 zilizopigwa, wabunge wote walipiga kura ya ndio kumuidhinisha Majaliwa kuwa mtendaji  mkuu wa shughuli za Serikali.

"Idadi ya kura zilizopigwa ni 350, hakuna kura yoyote iliyoharibika, kura ya hapana hakuna hata moja zote 350 zimemthibitisha Mhe.Kassim Majaliwa, kwa hiyo waheshimiwa wabunge Mhe, Kassim Majaliwa amethibitishwa na bunge hili kuwa Waziri Mkuu kamili".Spika Ndugai

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad