Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Burna Boy Aipiga Kijembe Album ya Davido "Album Imefeli"


Masaa machache kuelekea kuachiwa kwa album ya Davido #ABetterTime tayari album hiyo imeanza kupokea ukosoaji, ni kutoka kwa mwimbaji mwenzake wa Nigeria, Burna Boy.


Burna Boy ameonekana kuendelea kuitaka bifu yake na Davido kwani kupitia twitter jana aliandika 'Floppy Disk' tweet iliyotafsiriwa kama Album ya Davido #ABetterTime tayari imefeli.


Ni muendelezo wa mafahari hawa kurushiana vijembe ambapo hivi karibuni walitupiana maneno kupitia nyimbo zao, Davido alimchana Burna Boy kwenye ngoma yake 'FEM' yenye maana ya nyamaza kwa Lugha ya Kiyoruba.


Kwenye album ya Twice As Tall ya Burna Boy, pia Davido alipokea konga. Kupitia ngoma zake 'Way Too Big’ na ‘Nor Fit Vex.’ Burna alisikika akimchana Davido lakini pia kwenye 'Real Life' Burna alirusha dongo akisema, F*ck a good time..."

-

Kwanini ugomvi wao? Vita ya maneno kati yao ilianza Mei 4, 2020 baada ya Davido kudokeza kwamba album yake #ABetterTime itaachiwa Julai mwaka huu, mwezi ambao pia Burna Boy aliahidi album yake #TwiceAsTall itatoka.


Baada ya hapo, Burna Boy alishindwa kuvumilia na kuamua kuandika kwenye insta story yake,

"July will be very funny, and I shall laugh accordingly" hii ilimfanya OBO kuamka naye na ku-post picha ya kutengeneza ikimuonesha akiwa na Wizkid kisha kuandika “The two greatest of all time, no cap."

-

Vyanzo vinaeleza pia mvutano wao ulichochewa pia na sakata la Burna Boy kushindwa kumpa 'credit' mwimbaji Peruzzi kwa kuandika wimbo wa 'Pull Up' ambapo Davido alitoka na kumchana Burna kwa kumnyima Peruzzi nafasi ya kuwa nominated kwenye tuzo za Grammy kwa sababu wimbo huo ulikuwa kwenye album ya 'The African Giant' ilyowania Grammy 2019.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments