11/13/2020

Cardi B Amejikuta Kwenye Wakati Mgumu wa Kukoselewa Baada ya Kutumia Muonekano wa Mungu wa Kike wa Wahindi

 


Cardi B amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kutukanwa na kukosolewa vikali na jamii ya Wahindu mara baada ya kutumia muonekano wa Durga, ambaye kwao ni mungu wa Kike (Hindu Goddess)


Cardi B aliubariki ukurasa wa mbele wa Jarida la Footwear News kwa picha zenye muonekano wa mungu huyo wa Kihindu, ambapo baadaye alijikuta akikalia kuti kavu kwa Wahindu kumkosoa wakidai anamdhalilisha mungu wao na ameingilia masuala ya kidini.


Jarida hilo pamoja na Cardi B walikuja na kuomba radhi, Cardi ameeleza kwamba

 

"Wakati nafanya photoshoot kwa ajili ya viatu vya Reebok, watu wa ubunifu waliniambia kwamba nitaenda kumuwakilisha mungu wa Kike (Hindu Goddess) ambaye ni ishara ya nguvu, Uanamke na ukombozi. Na hicho ndio kitu nikipendacho. Na japo ilikuwa poa, lakini kama kuna watu wanafikiri nimeidhihaki dini yao au Utamaduni wao basi nasema Samahani. Hiyo haikuwa dhamira yangu." alieleza Cardi B.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger