CCM watakiwa kuvunja makundi uchaguzi unapokamilika
Na Timothy Itembe Mara.
Wagombea na wapiga kura  katika nafasi ya mwenyekiti na makamu wa halmashauri za Tarime vijijini na mjini ndani ya Chama cha mapinduzi wametakiwa  uchaguzi ukimalizika kuvunja makundi.

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge viti maalumu,Ghati Zefania Chomete kwenye kikao kilichoondaliwa kwa ajili ya kuwapata viongozi nafasi ya wenyeviti na makamu wa halmashauri za Tarime uchaguzi ambao ulitarajiwa kufanyika jana ila kwasababu zilizonje ya uwezo  ulihairishwa hadi hapo baadae utakapoitishwa tena.

Mkutano huo ulikalia ukumbi wa Ofisi za Chama cha mapinduzi CCM wilayani hapa na kuhudhuriwa na Mwita Mwikwabe Waitara mbunge wa Tarime vijijini na Michael Mita Kembaki Mbunge wa Tarime mjini ambapo Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwaasa  wagombea na wapiga kura kuvunja makundi baada ya uchaguzi ili kudumisha heshima ya Chama.

“Mimi niwatake wagombea na wapiga kura kwa ujumla uchaguzi ukimalizika vunjeni makundi kwa sababu bila hivyo mnawapa wapinzani nafasi ya kuwasema na kuwatia udhaifu”alisema Chomete.

Mbunge huyo aliongeza kuwa kuvunja makundi kuna nafasi kubwa yakuwaletea wananchi waliowachagua  maendeleo na kuendelea kukumbatia makundi hakuleti maana ya maendeleo kwa jamii iliyowachagua ili kuwatumikia.

Kwa mjibu wa Katibu wa Chama cha mapinduzi,Khamis Mkaruka Kura aliwataja waliokuwa wakigombea nafasi kwa Tarime vijijini kuwa ni Godfrey Kegoye Diwani mteule kata ya Matongo,John Bosco Mbusiro kata ya Regicheri na Samwel Kiles Kata ya Nyakonga wakati huo huo wagombea ndani ya halmashauri ya Tarime mjini ni pamoja na Daniel Komote diwani mteule kata ya Nkenda ambaye anaomba nafasi ya mwenyekini,Daud Wangwe na Mseti Gotora.

Kura aliwataka madiwani kuchagua kiongozi atakaye endana na kasi ya Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli na kusimamia Ilani ya Chama cha mapinduzi 2020-2025.

Naye Diwani mteule kata ya Bumera,Degratius Ndege ambaye anagombea nafasi ya makamu mwenyekiti aliwataka wajumbe madiwani watakapo apishwa kutenda kazi kama walivyoomba kwa wananchi.

Ndege aliwataka madiwani pindi watakapoaapishwa kusimamia utekelezaji wa miradi pale ambapo wataungana na kuwa kitu kimoja ndani ya halmashauri huku wakiikosoa halmashauri inapowezekana.

Wakati huo huo diwani mteule kata ya Turwa  halmashauri ya Tarime mjini,Chacha Msukuma aliomba wagombea kuzingatia kile walichoomba kwa wananchi kuwa ni kuwaletea maendeleo na sio vinginevyo.

Msukuma alimaliza kwa kusema kuwa kuomba nafasi ni rahisi lakini kulinda nafasi inahatua nyingine kwa hali hiyo kwa yeyote ambaye hatakuwa amechaguliwa kwa wale ambao wanaomba nafasi za kuchaguliwa akubali yaishe.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments