11/12/2020

Chege Afunguka Alivyocheza na Rais Magufuli

 


Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani ambao wataongoza kwa miaka mitano ijayo umemalizika salama na kulikuwa na 'surprise' nyingi ambazo zimetokea wakati wa kampeni zikiendelea.

 

Moja ya surprise hizo ni Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwapa kofia baadhi ya wasanii na kucheza muziki pamoja, Chege Chigunda ni mmoja wa wasanii waliopata bahati ya kucheza 'style' ya mapanga shaa na Rais huyo kwenye jukwaa moja.


 Akizungumza tukio hilo kupitia kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio Chege amesema kuwa  "Mheshimiwa alihama jukwaa la waheshimiwa akanifuata kumaliza show na mimi, wakati Rais ananifuata jukwaani nikazuiliwa ila yeye akasema niachiwe nikacheza naye" 


Aidha ameendelea kusema "Nimegundua watu wa siasa wapo mbali na muziki ila wanaupenda, hakuna lawama mpya kwenye siasa lawama zote zimetumika, mimi sina utaalam wa kugombea nafasi za siasa".

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger