Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Chui atembea umbali wa kilomita 3000 kutafuta jike la kumpanda

 


Ametembea mwendo mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa na chui nchini India kupata "makazi" katika hifadhi ya wanyamapori.

Mnyama huyo dume ambaye anafahamika na kwa jina maarufu Walker miongoni mwa maofisa wa wanyamapori, sasa ana miaka mitatu na nusu na alitoka katika hifadhi ya wanyamapori ya jimbo la Magharibi la Maharashtra mwezi Juni mwaka jana. Huenda alikuwa anatafuta chakula, mahali pengine pa kuishi au jike wa kuzaa naye.


Akiwa amevishwa kifaa maalum cha kubaini alipo shingoni, alitembea mwendo wa kilomita 3,000 sawa na (maili 1,864) kupitia wilaya saba za Maharashtra na jimbo jirani la Telangana kwa zaidi ya miezi tisa na hatimaye "kutulia" katika hifadhi nyingine mjini Maharashtra mwezi Machi. Kifaa hicho kilitolewa katika shingo yake mwezi Aprili.


Hifadhi ya Dnyanganga iliyo na ukubwa wa kilomita 205 za mraba ni makazi ya wanyama wa kila aina. Lakimni Walker ndiye chui pekee anayeishi hapo, wanasema afisa wa wanayamapori.


"Hana tatizo la himaya yake. Na ana sehemu kidogo ya kutafuta chakula," Nitin Kakodkar, afisa wa ngazi ya juu wa katika jimbo la Maharashtra aliambia BBC.


Sasa maofisa wa wanyamapori wanatafakari uwezekano wa kumleta chui wa kike ili kumpatia Walker mwenza wa kuzaa naye, hatua ambayo huenda "isiyo ya kawaida".


Chui sio wanyama ambao unaweza kung'amua wanapotaka kuwa na jike , wanasema, na kwamba wana njia asilia ya kutafuta mke. Kando na hilo itakuwa vigumu sana kumhamisha chui kutoka hifadhi moja hadi nyingine.


"Sababu moja, ni kwamba sio hifadhi kubwa. Imezungukwa na mashamba na misitu iliyoharibiwa. Pia endapo Walker atazalia hapa, kutakuwa na changamoto ya kutafuta chakula hasa miongoni mwa chui wadogo ambao pia wataanza kutawanyika," Bw Kakodkar alisema.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments