Corona bado tishio, vifo vyake vyafikia milioni 1.3 duniani kote

advertise hereWakati matumaini ya chanjo ya virusi vya corona yakizidi kuongezeka, ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo, sasa umeua zaidi ya watu milioni 1.3, kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizokusanywa na AFP.Kwa ujumla, kuna watu 1,303,783 waliofariki kutoka watu 53,380,442 waliotangazwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo wa homa kali ya mapafu, maarufu kwa jina la Covid-19, ingawa wataalamu wanasema takwimu rasmi zinaweza kutaja sehemu tu ya idadi ya maambukizi na vifo.
Maambukizi mapya na vifo yameanza kuongezeka wakati kukiwa na wimbi jipya la mlipuko wa ugonjwa huo Ulaya na Marekani.
Karibu kifo kimoja kati ya vitano kinatokea Marekani, wakati Brazil inafuatia kwa kuangalia nchi zenye vifo vingi baada ya watu 164,737 kupoteza maisha, baadaye India (129,188), Mexico (97,624) na Uingereza (51,304).
Dunia ilishangilia habari wiki hii za mafanikio makubwa katika kusaka chanjo dhidi ya virusi hivyo vipya katika jamii ya corona, lakini wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Afya (WHO) walionya katika mahojiano na AFP dhidi ya upotoshaji na watu kupoteza imani.
Jijini Athens, Ugiriki imetangaza jana kufunga shule za msingi, chekechea na vituo vya kulea watoto kutokana na wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona kuongezeka.
“Serikali ya Ugiriki imeamua kufunga shule hadi Novemba 30,” inasema taarifa ya Waziri wa Afya Vassilis Kikilias.
“Hatukutaka kufunga shule za msingi. Hii ni hatua inayoonyesha hali ni mbaya kiasi gani,” aliongeza.
Shule za sekondarui zilishafungwa na masomo yote yanaendeshwa kwa njia ya mtandao tangu Jumatatu iliyopita.
Nchini Marekani, jiji la New York limefunga baa kukabiliana na wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona.Baa na klabu za usiku za Big Apple, iliyokuwa na maambukizi makubwa wakati mlipuko ulipoanza, ziliamriwa zifungwe saa 4:00 usiku na gavana wa jimbo hilo akaonya kuwa shule zinaweza kuanza masomo kwa njia ya mtandao kuanzia Jumatatu.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE