11/14/2020

Daftari la wapiga kura Uganda lapelekwa Uholanzi kuhakikiwa

 


Gazeti la Daily Monitor la Uganda linaripoti kuwa daftari la kitaifa la wapiga kura limepelekwa Uholanzi kwa ajili ya kuhakikiwa.Tume ya uchaguzi imeipa zabuni kampuni ya Uholanzi kuondoa majina ya watu walioandikishwa zaidi ya mara moja wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Januari.


“Tumeanza mchakato wa kuwathibitisha wapiga kura ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wanaostahili tu wanaonekana kwenye daftari na kwamba watapiga kura mara moja,” msemaji wa tume hiyo Paul Bukenya amenukuliwa akisema.


Haijulikani kama vyama vya siasa vilijulishwa kuhusu hatua hiyo.


Raia wa Uganda watapiga kura kuchagua rais na wabunge tarehe 14 mwezi Januari. Wagombea 11- akiwemo Rais Yoweri Museveni- watawania nafasi hiyo ya juu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

2 comments:

 1. Kichwa cha Habari si sahihi, Kina Ushabiki, Waandishi jiongezeni katika
  Taaluma na ubunifu on Neutrality katika
  Kuhabarisha. Kalamu yako inaweza kujenga au Kubomoa. Zingatieni Hilo.

  ReplyDelete
 2. Kichwa cha Habari si sahihi, Kina Ushabiki, Waandishi jiongezeni katika Taaluma na ubunifu on Neutrality katika Kuhabarisha. Kalamu yako inaweza kujenga au Kubomoa.

  Zingatieni Hilo.

  ReplyDelete

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger