Dkt. Mpango Aanza Kazi, Atoa Maagizo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAZIRI  wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa wizara yake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mapato na matumizi ya fedha za umma ili kufanikisha malengo ya maendeleo yaliyotolewa na Rais  John  Magufuli, wakati akizindua Bunge la 12.


Hayo aliyasema wakati akipokelewa katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba Jijini Dodoma baada ya kuteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo kwa mara ya pili, Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma.



Alisema kuwa bado kuna shida kubwa katika eneo la matumizi ya fedha za umma kwa kuwa fedha zinazopelekwa kutekeleza miradi mbalimbali hazitumiwi vizuri na kusababisha miradi mingine kutekelezwa chini ya kiwango.



“Tunahitaji jicho la pekee katika Halmashauri za wilaya na miji, tunapeleka fedha za miradi lakini mimi nakadiria kuna upotevu wa takribani asilimia arobani ya fedha hizo, kwa hiyo ni lazima tuwe na jicho kali ili kuokoa fedha za wananchi”, alieleza Mpango.


Amefafanua kwamba mpango wa kununua ndege, meli na vitu vingine katika kipindi cha miaka mitano itafanikiwa iwapo kila mmoja katika nafasi yake atasimama imara kuhakikisha mapato yanakusanywa na yanatumika kikamilifu.



“Watanzania wana matarajio makubwa kutoka katika Serikali yao hivyo watumishi wa wizara ambao ni kama kitovu cha maendeleo wanatakiwa kuhakikisha matarajio hayo yanafikiwa.



Dkt. Mpango amewashukuru watumishi wa wizara yake kwa utendaji kazi mzuri kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita lakini ameomba waongeze jitihada na maarifa katika kutekeleza miongozo mbalimbali ikiwemo hotuba ya rais ya kufungua Bunge la 12, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuweka mikakati madhubuti ya kufanikisha utekelezaji wake.



Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Dotto James, alimhakikishia waziri huyo kwamba menejimenti imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa ushauri wa kitaalam ili nchi iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad