11/17/2020

Donald Trump Awauliza Washauri Wake Uwezekano wa Kusishambulia IranRais wa Marekani, Donald Trump aliwauliza wasaidizi wake kuhusu uwezekano wa kuvishambulia vinu vya nyuklia vya Iran, miezi miwili kabla hajaondoka madarakani. Taarifa hizo zimeripotiwa jana na gazeti la New York Times. 

Kwa mujibu wa gazeti hilo, wasaidizi wa ngazi ya juu wa Trump walimshauri kutofanya mashambulizi, wakimueleza kwamba hatua hiyo inaweza kusambaa na kuwa mzozo mkubwa katika wiki zake za mwisho za urais. 


Mkutano huo uliofanyika siku ya Alhamisi katika Ikulu ya Marekani, ulitokana na taarifa za Shirika la Kimataifa la kudhibiti matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA kwamba Iran imeongeza kurutubisha madini ya uranium mara 12 zaidi ya kiwango ambacho kinaruhusiwa katika makubaliano na mataifa makubwa yenye nguvu. 


Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, Kaimu Waziri wa Ulinzi Christopher Miller na Mwenyekiti wa baraza la kijeshi, Mark Milley

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger