Drake Aamba Shavu Nono...Kucheza Filamu Akiigiza Maisha ya Rais wa Marekani Barack Obama


Drake ana mihuri yote toka kwa Barack Obama, kwa ajili ya kucheza filamu ya maisha yake. Rais huyo namba 44 wa Marekani amezungumza na Complex na kumpa baraka zote OVO, kuvaa uhusika wake kwenye filamu.


"Nitasema hivi, Drake anaonekana kuwa tayari kufanya chochote anachotaka. Nikimaanisha ni mtu ambaye amebarikiwa kipaji. Kama muda ukifika, na akiwa tayari, basi Drake ana mihuri yangu yote ya kumpitisha. Ninahisi Malia na Sasha watafurahishwa nalo." alizungumza namba 44.


Drizzy aliwahi kutuambia nia yake ya kutaka kucheza uhusika wa Barack Obama kwenye filamu itakayohusu maisha yake. Kwenye mahojiano na Paper Magazine mwaka 2010 alizungumza hayo.


Ni staa gani wa bongo ambaye unaona ataweza kuuvaa uhusika kwenye filamu ya maisha ya Rais mstaafu wa Awamu ya 4, Jakaya Mrisho Kikwete?


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments