Edo Kumwembe Afunguka Sakata la Mbwana Samatta na Ston Villa "Mbwana Samatta Hakutaka Kuondoka"


Miongoni mwa taarifa zilizowashtua na kuwaumiza Watanzania wengi ni ile ya mchezaji Mbwana Samatta kuihama Aston Villa na kutimkia Fenerbahçe ya Uturuki mara baada ya kuitumikia Villa kwenye michezo 16 pekee.


Wengi waliitupia lawama Klabu hiyo ya Ligi Kuu nchini England kwa kusema hawakutenda haki kwa nyota huyo ambaye aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza England, pia kundi lingine la Watanzania lilimtupia zigo la lawama 'Samagoal' kwamba alishindwa kukaza.

Sasa mchambuzi wa Soka nchini Tanzania Edo Kumwembe (@edokumwembe) kwenye mahojiano na Kipindi cha #SalamaNa wiki iliyopita alieleza kinaga ubaga hadi Samatta kutimkia Uturuki

"Kwa ninayo sikia kwa sababu kwa bahati mbaya sijawahi kuongea na Samatta kuhusu hili, lakini kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya kuaminika ni kwamba yule Boss aliyekuja Mkurugenzi wa Ufundi alitaka watu wake ili naye apate deals kwa kuingiza wachezaji wapya. Kwa hiyo kuna wachezaji lazima watolewe sadaka, mmoja wapo akawa Mbwana Samatta." alisema Edo na kukazia kuwa uamuzi ule haukuwa sawa kwani timu yote ilikuwa chini ya kiwango na sio Samatta pekee.

Aliendelea, "Mbwana Samatta hakutaka kuondoka, Fenerbahçe walitumia nguvu sana na walimtumia hadi ndege binafsi (private jet) kumpeleka Uturuki. Na nilichosikia wanamlipa mara Tatu au mara Nne zaidi ya Aston Villa kile walichokuwa wanamlipa. Niliwahi ku-chat naye kidogo, ndoto yake kubwa bado ni kucheza England. Kwa hiyo sio kwamba alitaka ni wao ndio hawakumtendea haki." alimaliza Edo na kukazia kwamba ilibidi wamuhukumu msimu huu kwani msimu uliopita alicheza michezo 16 na kufunga bao 2, ukizingatia aliukuta msimu katikati na hakushiriki Pre-Season na wenzake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments