Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Esma Akiri Ndoa Yake Kuweka Rekodi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREUSIKU ule wa Agosti Mosi, mwaka huu, hakuna mwenye roho nzuri ambaye hakutoa neno la hongera kwa mwanamama Esma Khan almaarufu Esma Platnumz alipokuwa akisherehekea kufunga ndoa yake ya tatu na mfanyabiashara tajiri wa jijini Dar, Yahaya Msizwa.


 


Esma ni mwanamama, mjasiriamali na maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), lakini pia ni dada wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.


 


Sherehe ya ndoa yake hiyo ya kifahari iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 300 ilifanyika kwenye Ukumbi wa Lugalo Golf uliopo Mwenge jijini Dar na kuweka rekodi ya ndoa ya kifahari zaidi iliyofungwa mwaka huu nchini Tanzania.


 


Mastaa wengi wa Kibongo kutoka tasnia tofautitofauti za burudani hawakusita kumpongeza Esma kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram kutokana na umaarufu wake.


 


Pamoja na kwamba, wengi walikuwa wanafahamu uhusiano wake na meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Ahmed Hashim ‘Petit Man’ aliyezaa naye mtoto mmoja wa kike aitwaye Taraj, lakini aliyefunga naye ndoa ni mwingine kabisa ambaye wengi hawakudhani na wala hawakuwa wakimfahamu.


 


Hata hivyo, wapo waliokwenda mbele zaidi na kutafuta undani wa mwanaume huyo ndipo wakaibuka na habari za ndani kwamba alikuwa na wanawake wawili hivyo Esma aliolewa mke wa tatu.


 


Inafahamika kwamba, Esma ana maadui wengi waliompachika jina la Yuda-Isikarioti kutokana na kuwageuka wapenzi wa kaka yake, Diamond au Mondi pale wanapoachana na jamaa huyo hivyo waliibuka na kauli isemayo; “Wataachana tu!”


 


Kama hao maadui zake walivyotabiri ndivyo ilivyokuwa kwani miezi mitatu baadaye, hatimaye Esma anakiri ndoa yake kuweka rekodi ya kuvunjika mapema zaidi, ingawa zipo zilizoweka rekodi zaidi yake.


Esma anasema kuwa, ameamua kuachana na Msizwa kwa sababu jamaa huyo siku hizi amekuwa ni mtu wa mitandao tofauti na zamani, jambo linalomkera mno.
“Unajua mimi wakati ninaolewa na Msizwa, nilimpendea kitu kimoja, alikuwa siyo mtu wa mitandaoni kabisa; yaani hata alipokuwa anaona ninapiga picha, yeye anakaa pembeni, hataki aonekane.


 


“Lakini siku hizi Msizwa amekuwa ni mtu wa mitandaoni sana, inafikia hatua ana-dm (kutuma meseji za moja kwa moja) mpaka kurasa za udaku ili watoe habari zake na mimi. Akiamka asubuhi, saa kumi na moja, unamkuta yupo Instagram. Hayo maisha yamenishinda, ndiyo maana nimeamua kuachana naye,” anasema Esma.


 


Kwa upande wake, Msizwa alikaririwa akisema kuwa, hajamuacha mke wake huyo ila yupo safarini kwa ajili ya mambo yake ya kikazi.


“Nipo safarini kwa sababu ya kazi, lakini pia huku kuna familia yangu, anavyosema kuwa mimi nimekuwa mtu wa mitandaoni siyo kweli kwa sababu mimi ninatumia Instagram muda mrefu sana, sasa kwa nini kipindi hiki ndiyo ije inibadilishe?


 


“Halafu mimi sijamuacha Esma kwa sababu sijampa talaka yoyote na wala sijaposti talaka sehemu yoyote ile,” alikaririwa Msizwa.


Kabla ya ndoa hiyo ya tatu na Msizwa, Esma alitengana na Petit Man na kabla ya hapo alikuwa ameolewa na mwanaume mwingine ambaye alizaa naye mtoto mmoja hivyo kwa sasa ni mama wa watoto wawili.

Post a Comment

0 Comments