Fahamu jicho lenye maana ya siri linaloshirikishwa na Iluminati

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Dhana ya uwepo wa kitu cha siri imeghubika nembo za kwenye sarafu na kufanywa kuwa ishara au alama inayoonekana.

Alama ya ‘Jicho’ – hili ni jicho ndani ya umbo la pembe tatu – ni moja ya alama inayohusishwa na masuala ya ushetani ambayo pia imeonekana kuwa na uhusiano wa karibu na Iluminati, kundi la watu matajiri linalosemekana kwamba hutafuta kumiliki mali za dunia kwa nguvu ya shetani.

Alama hii ya jicho inadhaniwa kuficha kitu fulani kwasababu yenyewe ipo sehemu fiche kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kuitambua kwa macho yake moja kwa moja.

Pia inajitokeza sio tu kwa makanisa kadhaa bali pia kwenye majengo yenye kujihusisha na imani za kishetani kote duniani na pia alama hiyo ya jicho ipo katika noti za dola za Marekani pamoja na chapa ya muhuri mkubwa wa Marekani.

Ukweli ni njia ya zamani isiyo ya kawaida ya kuashiria nchi. Na alama ya jicho inaashiria matamanio ya kuwa na sauti au nguvu.

Ukichanganya na lile umbo la piramidi, ni kama ishara ya kundi fulani la zamani.

Lakini-kwanini-watu-hulinganisha-alama-hii-na-masuala-ya-ushetani”

Mchoro wa Pontarmos unashirikisha Jicho lenye maana ya siri

Awali kabisa, alama hiyo ya jicho ilikuwa na Kikristo na matumizi ya kwanza kabisa ya alama hiyo yanahusishwa na michoro ya dini hasa ya kumwakilisha mungu

Ilibuniwa kama ishara ya uangalizi wa huruma ya Mungu juu ya wanadamu.

Chanzo kingine cha alama hiyo ni kitabu cha zamani kabisa cha nembo ambacho kwa mara ya kwanza kabisa kilichapishwa mwaka 1593. Alama hiyo ya jicho iliwekwa kuashiria ‘utakatifu’ yaani ‘mungu’.

Kujenga-yaliopita

Hakuna anayejua chanzo cha ubunifu wa alama hii lakini wa kwanza kabisa kuhusika na ubunifu wake aliihusisha na imani za kidini.

Umbo la pembe tatu lilikuwa ni alama ya muda mrefu ya Utatu wa Kikiristo; yaani Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; na kuna wakati Mungu aliashiriwa kuwa ndani ya umbo hilo la pembe tatu.

Miale ya mwanga ambayo mara nyingi hungaa ndani ya alama hiyo pia ni miongoni mwa alama za mwanzo kabisa za Kikiristo.

Lakini chanzo cha lile jicho ni nini? Mungu amekuwa akiashiriwa kwa njia nyingi hapo kabla, mfano mkono mmoja unaojitokeza kutoka mawinguni lakini sio kama jicho.Katika kitabu cha Hours, Mungu alionyeshwa katika kifaa chenye pembe tatu kikimaanisha Baba, Mwana na roho mtakatifu

Katika kitabu cha Hours, Mungu alionyeshwa katika kifaa chenye pembe tatu kikimaanisha Baba, Mwana na roho mtakatifu
Pengine itakuwa sawa kwa pande zote kusema kuwa jicho hilo kuoneshwa peke yake lina athari yake kisaikolojia inayoonesha mamlaka.

Unaweza hata kuona athari hii kwa hali halisi mfano baadhi ya wanyama wana alama za jicho kwenye ngozi zao kama njia ya kuogopesha wanyama wawindaji.Kio cha Magrittes

Lakini pia kuna historia ya muda mfrefu sana inayoghubka alama ya jicho ambayo inaturejesha hadi nyakati za dini za wakati huo.

Karne ya tatu, Wasimeria walionesha utakatifu wa michongo fulani kwa kuchonga jicho likiwa kubwa zaidi ili kuongeza ile nakshi ya kuonesha ni miungu.

Pia walikuwa na sherehe ambapo wasanii walifanya michongo ya masanamu kuonekana kuwa na uhali kwa kufungua macho ya masanamu.Metropolitan Museum of Art

Siku za kale Misri ndio waliokuwa chanzo cha alama yenye kuhusishwa na jicho hilo kama mchoro: kwa mfano, macho mawili yalichorowa kwenye jeneza kwa imani kuwa yalimuwezesha aliyekufa kuona katika maisha yake baada ya kifo.

Na moja ya michoro maarufu nchini Misri ni ‘Jicho la Horusi’ ambalo lilikuwa linaashiria, ulinzi, afya njema na madaraka.

Kulingana na elimu ya visasili yaani kuhusu miungu na viumbe wa kale nchini Misri, miungu mfalme Horusi ambaye mara nyingi alioneshwa kama ndege Kozi- kipanga, macho yake yalitolewa akiwa vitani na timu ya mjombake. Lakini kwa usaidizi wa Mungu wa Kimisri ‘Thothi’ aliweza kuona tena.

Hivyo basi, Macho ya Horusi yalichukuliwa kama alama ya kujilinda, mchongo mdogo tu ambao ulikuwa unaweza ukaingizwa hata kwenye mfuko wa nguo uliovaa kama njia moja ya kujilinda.Jicho la Horus lilitumiwa kama mfumo wa ulinzi

Mchoro huu na mingine ilikuwa na athari kwa nchi za Ulaya. Tatizo kubwa wakati huo ikiwa ni kuchukua michoro na kuifasiri visivyo kwasababu hawakuelewa maana halisi ya michoro wenyewe.

Na alama ya jicho inasemekana kuna uwezekano mkubwa ilifika mahali ikafasiriwa visivyo.

Karne ya 18, ndio fasiri ya alama ya jicho inaaminika kuwa ilibadilika pakubwa.

Baada ya mapinduzi kwaka 1789, katika azimio la Haki za Raia kulikuwa na alama ya jicho kwa juu.

Uingereza mwaka 1794, Jeremy Bentham alimuagiza msanifu ujenzi Willey Reveley kutengeneza nembo ya gereza jipya na jengo hilo likawa na nembo ya jicho – ishara ambayo sasa hivi imezungukwa na maneno ‘Huruma’, ‘Haki’ na ‘Uangalifu’.Jicho la Providence linaonekana katika tangazo la haki za mwanamume na raia 1789

Miaka michache nyuma, Mwaka 1782, Muhuri mkubwa wa Marekani ulizunduliwa ambao ulikuwa na alama ya jicho ishara iliyolengwa ikiwa ni ‘Mungu kuwa na huruma’ kwa taifa hilo.

Hili ni dhihirisho tosha kwamba alama hiyo haikuwahi kuhusishwa na kuabudu shetani

Sasa je ilikuwaje hadi alama hiyo ikaanza kuhusishwa na Iluminati?
Taarifa za chimbuko la kundi hilo bado haziko wazi lakini inasemenaka kuwa liliundwa mwaka 1776 na kuvunjwa 1787 na pia ni kweli kundi la Iluminati lilivutiwa na alama ya jicho na kutaka kuitumia kuashiria ‘Nguvu ya Mungu’ wakati huo.

Ingawa, kundi la ushetani la ‘Mason’ halikutumia alama hiyo hadi mwishoni mwa karne ya 18. Kwa bahati mbaya dhana nyingi zilizopo zinazungumzia uzuri wa alama ya jicho wala sio siri za viongozi wanaojihusisha nayo.

Na katika siku tunazoishi, wanamuziki kama Madonna, Jay-Z na Kanye West wote wamewahi kushutumiwa kujihusisha na kundi la Iluminati ikiwemo matumizi ya alama au ishara ya Jicho.

Utumiaji wa alama hii umeonekana hata kwa wasanii wengine zaidi kama Bentham, Le Barbier, Thomson, Barton na wengine wengi hivyo basi sio ushahidi tosha kuwa alama ya jicho inahusishwa na ushetani lakini pia inaweza kuwa nembo kama yoyote ile.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad