Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Familia: Mazishi ya Ginimbi hakuna sherehe
Familia ya bilionea wa Zimbabwe, Kadungure Ginimbi aliyefariki siku chache zilizopita imesema hakutakuwa na sherehe kwenye mazishi yake.

Mtandao wa Zimbabwe Cronicles umeripoti kuwa mwili wa Ginimbi utawasili nyumbani kwake alfajiri ya leo Jumamosi.


Kulingana na mtandao huo ndugu yake, Clement Kadungure ambaye alinukuliwa akisema kwamba, kutakuwa na ibada ya wafu ambapo watu wa karibu wa marehemu watazungumza.


Mwili wake baadaye utazikwa nyumbani kwake na sio ndani ya nyumba yake kama inavyoarifiwa na baadhi ya watu.


Kwa mujibu families hiyo, Ginimbi atazikwa kulingana na tamaduni za jamii yake.


Pia imekanusha madai kwamba kutakuwa na sherehe ya kuvaa mavazi meupe akisisitiza kwamba yatakuwa mazishi na sio sherehe na kwamba wanaotaka kuvaa mavazi hayo watafanya hivyo kwa hiari yao. Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments