Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

GEITA: Akamatwa na Polisi baada ya kumtoa mimba na kumsababishia kifo mwanamke wa miaka 40Jeshi la polisi mkoa wa Geita, linamshikilia Vestina Michael (44), mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kumtoa mimba na kumsababisha kifo Mariam Msalaba (40), ambaye alipoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa mimba nyumbani kwa mtuhumiwa.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Henry Maibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kitendo hicho cha kikatili kimetokea nyumbani kwa mtuhumiwa majira ya usiku.


“Jeshi la Polisi tunamshikilia Vestina Michael, kwamba siku ya Oktoba 31 mwaka huu marehemu alifia nyumbani kwake na ndugu wa marehemu wakaleta malalamiko kwamba, ndugu yao amefia kwa mtuhumiwa wakati akimtoa mimba, hivyo tunamshikilia huyo mtuhumiwa”, amesema Kamanda Mwaibambe.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments