Guardiola amgeukia Grealish, Lampard amng’ang’ania GiroudPep Guardiola anataka Manchester City kumsajili Jack Grealish, baada ya kubaini kiungo huyo wa kati wa Aston Villa na England, 25, kama kipaumbele chake katika mipango yake ya kuunda kikosi kipya. (Independent)

Jack Grealish

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anasisitiza mlinda lango Dean Henderson “anataka kusalia Manchester United”, licha ya ripoti kuwa mchezaji huyo wa kimataifa, 23, huenda

Kocha wa Chelsea Frank Lampard anasema mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, ambaye anataka kuhama  kutafuta fursa ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza kabla Ligi ya Ulaya kuanza mwaka ujao, ni “mchezaji muhimu” na amesisitiza anataka asalie Stamford Bridge. (Mirror)Olivier Giroud

Chelsea ina imani kuwa Giroud atasalia lakini hatamzuilia ikiwa mchezaji huyo wa Ufaransa atataka kuondoka. (Independent)

Real Madrid bado haijapokea ofa yoyote kwa ajili ya kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 28, ambaye amehusishwa na Manchester City na Arsenal. (AS)

Borussia Dortmund iko tayari kuanzisha tena mikakati ya kumsaka kiungo wa kati wa Inter Milan raia wa Denmark Christian Eriksen, baada ya kuhusishwa na mchezaji huyo, 28, aliyekuwa Tottenham mapema mwaka huu. Isco

Kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo ana imani kuwa wataanza kupata magoli – na kupunguza shinikizo kwa mfungaji mzuri wa magoli mshambuliaji raia wa Mexico Raul Jimenez, 29. (Express & Star)

Wakati huohuo Ole Gunnar Solskjaer amemuambia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 24, hawezi kutulia na tabia yake yote akiwa Manchester United baada ya mwanzo mgumu wa msimu kwa timu hiyo. (Mail)

QPR itamsaka tena beki wa kati na kumuuza mlinzi wa Jamhuri ya Ireland wa Under-21 Conor Masterson, 22, kwa mkopo dirisha la usajili litakapofunguliwa Januari. (West London Sport)Anthony Martial

Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish anakabiliwa na hatari kushtakiwa kwa kosa la nne la uendeshaji mbaya wa gari mwaka huu kulikotokea karibu na eneo la kufanya mazoezi la klabu hiyo mwezi uliopita (Birmingham Mail)


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments