GWIJI wa soka wa Argentina, Diego Armando Maradona, aliyefariki dunia juzi Novemba 25, amezikwa na watu wachache, jana Alhamisi Novemba 27 mjini Buenos Aires, pembeni ya makaburi ya wazazi wake.

 

Wanafamilia na marafiki wa karibu wa mchezaji huyo ndiyo walioruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yaliyokuwa chini ya ulinzi mkali.

 

Mashabiki walijipanga barabarani wakipeperusha bendera ya Argentina wakati gari lililobeba jeneza la Maradona likipita huku simanzi ikiwa imetanda kwa mashabiki hao wakiangusha vilio vizito.Huko Italia mashabiki wa timu ya Napoli walikusanyika nje ya uwanja wa timu hiyo, Stadio San Paolo, kuomboleza kifo chake.

 

Uongozi wa timu hiyo umesema utabadili jina la Uwanja huo  na kuwa Maradona Stadium kwa heshima ya lejendi huyo aliyecheza kwenye klabu hiyo kwa mafanikio makubwa kati ya mwaka 1984–1991.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments