Hajawahi Tokea..Rekodi ya Upigaji kura Mapema yavunjwa Huko Marekani huku Watu Milioni 90 Tayari Wakiwa Washapiga Kura

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


 Data nchini Marekani zinaonyesha kuwa rekodi ya upigaji kura mapema nchini humo imevunjwa baada ya watu milioni 90 kushiriki zoezi hilo la kumchagua rais kufikia sasa. 

Haya yamefanyika wakati Rais Donald Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic wakiwa wanafanya kampeni kote nchini humo kujaribu kuwavutia upande wao wapiga kura waliosalia ambao hawajaamua ni nani watakayempa kura yao. 


Idadi kubwa ya waliopiga kura mapema ikiwa ni asilimia 65 ya wapiga kura wote walioshiriki zoezi hilo mwaka 2016 inaonyesha jinsi kinyang'anyiro hicho kilivyo kikali huku zikiwa zimesalia siku tatu tu za kampeni. 


Hofu ya kuambukizwa virusi vya corona katika milolongo mirefu ya upigaji kura siku ya Jumanne ni mojawapo ya sababu zilizochangia pia kwa watu wengi kushiriki upigaji kura wa mapema. 


Kura za maoni zinamuonyesha Donald Trump akiwa nyuma ya Joe Biden kitaifa, lakini ushindani ni mkali katika majimbo muhimu ambayo ndiyo yatakayoamua mshindi wa uchaguzi huo

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad