"Hakuna wa Kuvunja Katiba, Hawana Sifa"- Msekwa

 


Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.

"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Mzee Msekwa, sina uhakika na mazingira
    yaliyojiri na mkomeshano uliojitokeza.

    Wabunge wateule wamekula kiapo wakiwa wanachama hai wa chama kilicho wapeleka na wana kesi yao katika mkomoano na udhalilishaji mahakamani ambayo ina toa mandate kuendelea na majukumu ya uwakilishi mpaka uamuzi wa mwanzo utakapo tolewa .

    Wataendelea na majukumu yao mpaka hapo

    ReplyDelete