Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Harmo, Kajala Mambo ni Moto!

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURETABIA ya kupe ni kuganda kwenye ngozi pale anapofyonza damu; unauliza mfano una maana gani kwenye stori hii, subiri upakuliwe ubuyu. Iko hivi; yale madai yaliyovuma miaka miwili iliyopita kuwa msanii wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na malkia wa filamu Bongo, Kajala Masanja wana ulimwengu wao yamezidi kuwaganda ambapo sasa inadaiwa kuwa mambo kati yao ni moto.


 


Chanzo cha karibu na wawili hao kilidai mbele ya mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Harmo kudaiwa kumwagana na mkewe Sarah Michelotti, kwamba msanii huyo amehamishia moyo wake kwa Kajala.


 


“Harmo kwa sasa yupo na Kajala, fuatilieni,” kilisema chanzo chetu na kushindwa kuweka vielelezo mezani juu ya ukweli wa tuhuma hizo. Hata hivyo, madai kuwa wawili hao wana mambo yao yalivuma mwaka 2018 baada ya kusambaa kwa kipande cha mwito wa simu wa video (video call) kikiwaonesha kuwa waliwasiliana huku kila mmoja akiwa amejiachia kitandani.


 


“Unaona unaona” zilipozidi kuwa nyingi kwao, Harmo alijitokeza mwaka huo na kukanusha, huku Kajala akijitokeza na kuonesha chuki juu ya yule aliyesambaza video hiyo ya siri.


 


Aidha, taarifa za uhakika zilionesha kwamba Jacqueline Wolper ambaye mwaka huo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmo alimaindi na inadaiwa Wolper na Kajala hawajawa na maelewano mazuri.


 


RISASI MCHANGANYIKO lilimtafuta Harmo kwa njia ya simu ili kumuuliza ukweli wa ishu hii ambapo simu yake iliita bila kupokelewa huku meneja wake Harmo, Beauty Mmari, mara kadhaa amekuwa akisema: “Mambo binafsi kuhusu Harmo siwezi kuyazungumzia, mtafuteni mwenyewe.”


 


Naye Kajala kama ilivyo kwa Harmo hakupatikana, lakini rafiki yake wa karibu alisema: “Jambo hilo linawezekana lakini kwa kuwa sina ushahidi endelea kuchunguza.”


 


Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu kupitia kwenye mitandao ya kijamii umeonesha kuwepo kwa tetesi hizo za Kajala na Harmo kufanya yao.


 


“Watu bwana, kuna ajabu gani kwa Harmo na Kajala kuwa wapenzi, waacheni wajiamulie mambo yao kama ninyi mnavyojiamulia yenu,” ilisomeka komenti mmoja mtandaoni. Aidha, mwandishi wetu alifanikiwa kuona baadhi ya kurasa za udaku zikiwa zimeposti tetesi hizo ambazo zinafanyiwa kazi na timu yetu uchunguzi.Post a Comment

0 Comments