11/01/2020

Hatiamye Mbowe Ataja Sababu Kukataa Matokeo ya Uchaguzi MkuuBy Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vyama vya Chadema na ACT- Wazalendo vimesema havitambui matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, ikiwa ni pamoja ushindi wa wagombea wao katika ngazi ya ubunge, udiwani na uwakilishi.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza John Magufuli kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano baada ya kupata kura milioni 12.5, huku chama hicho kikongwe kikitangazwa mshindi katika majimbo yote isipokuwa manane.


Pia tume ya Zanzibar, ZEC imemtangaza Dk Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais, huku ushindi wa chaguzi zote ukiweka rekodi.


Lakini leo Ijumaa (Oktoba 31), mwenyekiti wa Chadema, Freema Mbowe kwa niaba ya vyama vya ACT- Wazalendo na chama chake, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanapinga matokeo hayo.


“Sisi kama vyama tumesema uchaguzi huu hatuutambui na tunapoacha kuutambua ni kwa kuwa tumeridhishwa pasipo shaka kuwa matokeo yoyote, hata kama yametoa nafasi kwa mtu wa chama chetu, si matokeo yaliyo halali,” alisema Mbowe.


“Ni matokeo yaliyotengezwa kwa mkakati na makusudi ya kutugawa sisi. , hatutakubali kuwa washirika wa mapato yatokanayo na jinai.”

 

Alisema hawako tayari kufaidi matunda yatokanayo na uhalifu kwa madiwani, wabunge na wawakilishi wa Chadema na ACT. Uchaguzi hautambuliwi na huo ndiyo msimamo ambao wanaamini wapenda haki wataufuata


Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto kabwe amesema wamekwishakubalina kuwa hakuna diwani, mbunge wala mwakilishi wa vyama hivyo ambaye atakwenda kuapa na wanaamini kuwa hakuna atakayefanya hivyo.


“Chochote ambacho kitatokana na manufaa ya uharamu uliotokea, sisi hatutakubaliana nacho,” alisema Zitto aliyekuwa mbunge wa Kigoma Mjini. “Tunachokitaka ni mambo mawili marahisi sana; moja hapakuwa na uchaguzi tarehe 28, Oktoba, mbili tunataka uchaguzi mpya na uchaguzi huo uendeshwe na tume huru ya uchaguzi itakayoundwa kuendesha chaguzi zote kwa Zanzibar na Tanzania Bara.”


Zitto amesema madhara na chochote kitakachotokea hawatakibeba wao, bali watabeba waliofanya matokeo hayo, huku akisema matokeo yake ni mabaya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

3 comments:

 1. Ukweli ni kwamba, Faru Joni alizowea vya Dezo. Amekula RUZUKU SANA.
  AMEWACHAKACHUA WALIOMALIZA UBUNGE SANA

  Sasa kila Akiangalia mie na Genge langutunatokaje kwa Mbungo. anadhani
  labdaataweza kukiwakisha. HILO HALIPO

  KWA ASLAHI YENU WACHACHE NA UCHU WENU
  HAMTUINGIZI BARABARANI.

  MUNGU AMREHEMUAKWILINA AKWILINA, ULISHA SAIDIAAU KUWATEMBELEA WAZAZI WA
  MAREHEMU MWAKA HUU..? JIBU UNALO.

  MCHUKUE DEO NA DOKTA UKIONE CHAKO.

  MIE, SISI NA WALE HATUINGI KUKUTAFUTIA RUZUKU..MIE NAENDELEA NA BODABODA YANGU KUTAFUTA RIZIKI.

  YA MAANDAMANO NI YAKO NA FAMILIA YAKO

  ReplyDelete
 2. Mboowee, wewe toka lini?..ukawa msemaji
  wa Ndg. Menadi Kamelius Membe.

  Mungu alie juu. Kakuumbua kwa matendo
  yako Batili.

  WaTanzania tumeamua na kupaza Sauti
  Zetu Mahali muafaka na Siku muafaka ya 28 Oct.

  WALIO SAFIRI KUHAMASISHA NCHI ZA UGHAIBUNI WASITUPE MKOPO PIA TUMEMPUMZISHA. DAGAA NA MAWESE SAIZI YAKE.

  Amani yako ni muhimu kuliko Ruzuku uliizowea. Haiko, fanya kazi.

  ReplyDelete
 3. Mahaini nyinyi. Hapa mmebugi stepu.
  Siingii barabarani kukutafutieni Ulaji na Familia zenu.

  Tafuteni kazi halali mpate riziki iliyo halali Mna historia ya Dhuluma.

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger