Hesabu ya Ndoa Inambeba Zaidi Zari kwa MondiMWISHONI mwa wiki iliyopita gumzo kubwa lilikuwa ni ujio wa mwanamama mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ Bongo. Aliibuka akiwa ameambatana na watoto wake wawili aliozaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tiffah na Nillan.


 


Kilichowashtua mashabiki wengi ni kitendo cha mzazi mwenziye huyo wa Diamond au Mondi kuibuka nchini baada ya kipindi cha takribani miaka miwili kupita akiwa hana mawasiliano mazuri na mzazi mwenziye huyo tena bibie akiwa amejinasibu kabisa kuwa amemuacha Mondi kutokana na vitendo vya usaliti.


 


Mondi kabla ya kukutana na Zari, alishakuwa na wapenzi wengine akiwemo Miss Tanzania 2006, Wema Isack Sepetu. Wema na Mondi ni moja kati ya kapo pendwa sana iliyowahi kutokea hapa Bongo.


 


Watu waliwapenda sana wawili hawa walipokuwa pamoja. Sina shaka hata wao wenyewe kuwa wanapendana maana mara kadhaa, Wema alishathubutu kusema hadharani kwamba Mondi ni kati ya wanaume ambao wamegusa vilivyo uvungu wa moyo wake.


 


Vivyo hivyo kwa Mondi, naye alimpenda sana mlimbwende huyo. Kuonesha kwamba wawili hawa walikuwa wakipendana, mara kadhaa ilitokea waliachana lakini walijikuta wakirudiana baada ya kupita vipindi fulani fulani.
Mapokeo ya kapo yao yalikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii na hata magazeti Pendwa ambayo kimsingi ndiyo yalikuwa yakiwaandika sana. Familia ya mama Mondi kwa maana ya mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na wengineo, walimpokea kwa mikono miwili Wema.


 


Lakini pamoja na yote hayo, alipoingia Zari aliuvunja mwiko wa Mondi kurudianarudiana na Wema. Alijenga kibanda, akadumu kwa miaka ya kumtosha kabisa kuweza kumzalia watoto wawili. Zari akiwa tayari anao watoto wengine watatu kwa baba mwingine, akampa zawadi ya Mondi kuitwa baba kwa sababu mitandao ya kijamii na hata magazeti Pendwa ambayo kimsingi ndiyo yalikuwa yakiwaandika sana.


 


Familia ya mama Mondi kwa maana ya mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na wengineo, walimpokea kwa mikono miwili Wema. Lakini pamoja na yote hayo, alipoingia Zari aliuvunja mwiko wa Mondi kurudianarudiana na Wema.


 


Alijenga kibanda, akadumu kwa miaka ya kumtosha kabisa kuweza kumzalia watoto wawili. watoto wengine watatu kwa baba mwingine, akampa zawadi ya Mondi kuitwa baba kwa sababu Zari alikuwa bado analitumikia penzi lake kwa Mondi, Mobeto alipenya kwa siri na akakubali kuwa binti wa pembeni na utamu ukawakolea, wakapata mtoto mmoja. Kuna Mkenya anaitwa Tanasha Donna, naye aliichungulia fursa ya Mondi kuachana na Zari.


 


Akaweka alama kwenye maisha ya Mondi kwa kumzalia mtoto mmoja, akalala mbele na maisha yake licha ya kuwepo kwa taarifa za kutaka kuolewa. Hapo ndipo ambapo ukiangalia kwa makini utagundua hesabu zinambeba zaidi Zari kama ataamua kurejesha majeshi kwa Mondi.


 


Anayo bondi ya kukaa na kuwa na mafanikio zaidi na Mondi hususan katika suala zima la watoto na hata miaka waliyokaa kwa pamoja. Wema alikuwa anaingia na kutoka kama ilivyokuwa kwa mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ na warembo wengine wengi tu aliowapitia. Halafu kwa sasa, Mondi amekua. Ule ujana hawezi kuufanya tena kwani mbali na umri wake kumfunga lakini hata cheo chake, ni Mkurugenzi wa Wasafi Media.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE