Jinsi Trump anavyotumia mamlaka yake kutoutambua ushindi wa BidenKabla ya uchaguzi wa Marekani ,kuna maswali mawili yalikuepo kuhusu namna ambavyo rais Donald Trump atakubali kushindwa uchaguzi.


Swali la kwanza lilikuwa ni Je, Trump atakubali ushindi wa mpinzani wake wa Democratic Joe Biden.


Tayari tunajua jibu: Trump amekataa kukubali kuwa Biden ameshinda na kudai kuwa waliiba kura, bila kuonesha ushaidi wowote.


Swali la pili, lilikuwa ni kama rais atatumia mamlaka yake kuzuia kutambua ushindi wa Biden.


Na jibu linaanza kuonekana wiki hii, hatua kadhaa za utawala wa Trump kuhoji kuhusu matokeo ya uchaguzi na kuweka ugumu katika kupokezana mamlaka.


Katika mapambano haya ya matokeo ya uchaguzi , Trump amefanikiwa kuugwa mkono na viongozi wa chama chake cha Republican , ambapo maseneta wachache ndio walimpongeza Biden.


Baadhi ya wataalamu wa matukio ya namna hii, wanasema kuna hatari ya makabidhiano ya utawala yasiwe ya kawaida Marekani.


"Mambo yataendaje? Hakuna anayefahamu . Ingawa itategemea na wanachama wenzake wa Republicans kumsukuma Trump aondoke madarakani.


Lakini anaweza kuanzisha mgogoro katika katiba, anasema muandishi wa BBC Joshua Sandman, Profesa wa siasa ya sayansi kutoka chuo kikuu cha New Haven ambaye ni mtaalamu wa uchaguzi wa Marekani.


"Ni aibu "


Siku ya Jumanne, Biden alisema kuwa ni jambo la aibu kwa Trump kukataa matokeo ya uchaguzi , lakini kikosi chake kinaendelea na utaratibu wa kupokea mabadiliko ya utawala.


Makadirio ya ushindi wa Biden yanaonesha wazi kuwa chama cha Democrat kimepata ushindi wa kishindo kwa kura za wajumbe 270 katika uchaguzi ambapo Desemba 14, watamchagua rais wa Marekani ajaye.


Licha ya kwamba vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuhusu suala hili na viongozi wengine duniani wamempongeza Biden katika ushindi wake, Trump aliamua kupinga matokeo hayo kisheria.


Jumatatu, Mwanasheria mkuu wa Marekani William Barr alikubali kitengo cha haki kuchuguza madai hayo kama ya ukweli na yanaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi wa jimbo lolote.


Hatua hiyo haikuwavutia kundi la Trump pekee kuendelea kuonesha matokeo ya uongo, lakini ni kawaida kwa majimbo kufanyiwa uangalizi huru bila kuingiliwa na serikali iliyopo madarakani.


Na uamuzi wa Barr unaweza kusababisha kujiuzulu kwa afisa wa ngazi ya juu ambaye alisimamia uchunguzi huo, Richard Pilger.


Waziri wa mambo ya nje,Mike Pompeo pia alizua taharuki Jumanne baada ya kudai kuwa anategemea awamu ya pili ya uongozi wa Trump utaenda vizuri," bila kufafanua kama alikuwa anawatania waandishi wa habari au la.


Kwa upande mwingine timu ya Biden katika harakati za kumpitisha kwenye mamlaka iliripoti kuwa serikali ya shirikisho inawakwamisha na afisa aliyeteuliwa na Trump, Emily Murphy.


Murphy , kiongozi katika utawala ambao unaidhinisha kuanza kwa taratibu za kukabidhiana na amekuwa anakwepa kufanya taratibu zozote kwa kuwa Trump anapambania matokeo ya uchaguzi katika upande wa sheria bado.


Wanachama wa kundi la Biden wamesema kuwa amekuwa anawazuia hata kupokea simu kutoka kwa viongozi wa kigeni na kudai kuwa sheria itafuata mkondo wake.

 


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE