KAGERA: Mtoto wa miaka mitatu anusurika kufa baada ya nyumba kuteketea kwa moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, Okechi Onesphalis, mkazi wa eneo la Bunena, mkoani Kagera, amenusurika kifo baada ya nyumba aliyokuwa amelala kuteketea kwa moto jana jioni Novemba 8, 2020, akiwa ndani peke yake, wakati mama yake mzazi akiwa nje akiendelea na shughuli za utafutaji mali.

 

Wakizungumza na EATV wananchi wa eneo la Bunena katika Manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, wameeleza kuwa walifanikiwa kuokoa maisha ya mtoto huyo aliyeachwa peke yake akiwa amelala.


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, wamesema kuwa mtoto huyo aliachwa na mama yake akiwa amelala na kuwa wakati nyumba hiyo ya kupangisha iliyokuwa na familia sita, wakati inaanza kuteketea hata majirani wa mama huyo hawakuwepo.


Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera, Hamis Dawa, amesema kuwa mtoto huyo amepata majeraha ya moto na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa, huku akiwatupia lawama wananchi kwa kuchelewa kutoa taarifa pindi ajali za moto zinapotokea.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad