Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kagere, John Bocco Wawashika Pabaya Yanga
WASHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco na Meddie Kagere, wamewashika pabaya wapinzani wao Yanga kutokana na uimara wa safu yao ya ushambuliaji ambayo imeonekana kufanya vizuri katika mechi 10 ilizocheza hadi sasa.

 

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo inaongozwa na Kagere na Bocco, imefanikiwa kufunga mabao 22 hadi sasa ikiwa ni tofauti ya mabao 10 na wapinzani wao Yanga ambao wametupia kimiani mabao 12 huku ikiwa nafasi ya pili ya msimamo wa ligi.

 

 

Simba kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kwa kushinda mechi sita kati ya 10 ilizocheza, huku ikipoteza michezo miwili na kutoa sare mbili.

 

 

Kagere na Bocco ndio vinara wa mabao ndani ya Simba ambapo wote kwa pamoja wamefanikiwa kufunga mabao nane ambapo kila mmoja akifunga manne. Yanga kinara wao wa mabao ni Michael Sarpong ambapo ana mabao matatu, wanaomfuatia ni beki Lamine Moro na kiungo Mukoko Tonombe ambao kila mmoja ana mabao mawili.

 

 

Msimu uliopita Kagere alifanikiwa kuibuka mfungaji bora akifunga mabao 22 ikiwa ni mara ya pili mfululizo kutokana na msimu wa 2018/19 kutwaa tuzo hiyo akifunga mabao 23.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments