Kauli ya BAVICHA kwa Kamati Kuu CHADEMA juu ya walioapishwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limeishauri Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza uanachama, wanachama 19 waliokwenda kinyume na msimamo wa chama hicho, kwa kukubali uteuzi wa ubunge viti maalumu.


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee.

Hayo amesema Mwenyekiti wa Bavicha, John Pambalu leo Novemba 26, 2020, wakati anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo alitoa msimamo wa baraza hilo, baada ya kamati tendaji kukutana katika mkutano jana usiku Jumatano kwa njia ya mtandao kujadili wanachama hao 19 waliokwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum.

Akitangaza maazimio ya kamati tendaji hiyo ya Bavicha, Pambalu amesema, baraza hilo linaishauri kamati kuu hiyo ya Chadema kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge hao viti maalumu.

“Ziko adhabu nyingi za kuchukuliwa kwa hao 19, kuvuliwa nyadhifa zao, kunyang’anywa uanachama wao, dhambi ya usaliti ni dhambi mbaya, hatutaki kushinikiza Kamati Kuu ichukue hatua gani, lakini hatua kali zichukuliwe ikiwemo kuwafukuza uanachama wao, “amesema Pambalu.

Ameongeza kuwa, “Siku zote wasaliti ndani ya Chadema si mahala salama kwa wao, wanaweza  kuchagua kwenda katika chama ambacho usaliti ni kawaida, chama chetu usaliti si kosa la kawaida”.

Wanachama hao 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee, waliapishwa kuwa wabunge viti maalumu na Spika Job Ndugai, tarehe 24 Novemba 2020, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pambalu umepampalukia wapi.?

    Msaliti amesha sepa Nchi, baada ya kuona Watu hawakumwaga Damu kwa Uhamasishaji wake batili.

    Waache Wabunge wetu Wateule Walitumikie Taifa letu.

    Na wewe kama unataka ku Pambalu Ka, hakikisha unayo pasi poti yenye miezi isiyopungua 8.

    Wewe ni cha ndimu ktk Siasa. NYAMAZA.!

    ReplyDelete

Top Post Ad