Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kauli ya Solksjaer juu ya Hatma ya Kibarua Chake

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjaer amesema makosa yaliyofanywa na mabeki wake yaliyosababisha wafungwe bao 2-1 na Instanbul Basaksehir katika ligi ya mabingwa Ulaya si ya kusameheka.Mfungaji wa bao la kufutia machozi la Manchester United, Antony Martial (Aliye katikati), akirejesha mpira katikati ya uwanja.


Mabeki wa United walifanya makosa ya kizembe yaliosababisha Edin Viska na Demba Ba kufunga mabao yaliyowapa ushindi Instanbul ushindi wa kwanza katika ligi ya mabingwa Ulaya.


Akizungumzia mchezo huo, Solksjaer amesema ni mbaya sana kuruhusu mabao ya aina ambayo ni wazi yalikuwa makosa yasiyovumilika, na ameahidi watayafanyia kazi.


Katika hatua nyingine Solksjaer amezipuuza fununu zinazodai kwamba kazi yake ipo mashakani kutokana na mwenendo wa timu yake huku akisisitiza kwamba ameajiriwa kutekeleza majukumu yake na anajitahidi kadiri iwezekanavyo huku akiamini uwezo wa wachezaji wake.


Wachezaji wa zamani wa The Red Devils akiwemo aliyekuwa nahodha Roy Keane amekuwa wakikosoa mwenendo wa timu hiyo lakini Ole Gunnar amesema hiyo ni kazi yake na yeye anaendelea na kazi ya aliyokabidhiwa.

Post a Comment

0 Comments