Kauli ya Zitto Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa Z’barKIONGOZI Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema, hadi sasa chama hicho hakijafanya uamuzi kuhusu ushiriki wake katika uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

 

Zitto amesema uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo utatolewa katika vikao vya chama, kikiwemo cha Kamati Kuu  ambayo itaketi hivi karibuni.

 

Siku chache zilizopita, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi alisema ameacha nafasi za mawaziri kwa ajili ya ACT-Wazalendo, akieleza alipeleka barua kwa chama hicho ili kiwasilishe majina ya watu wake.

 

Zitto amesema chama chake hakikufanya makosa kuipokea barua hiyo, lakini kupokelewa kwake haimaanishi wamekubaliana na matakwa ya Mwinyi ya kukitaka chama kiwasilishe majina.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments