Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kaze Atoa DK 20 za Kuiua Simba Jumamosi

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Kocha Cedric Kaze, amewaambia vijana wake kuwa, katika mchezo wa keshokutwa Jumamosi dhidi ya Simba, anataka bao ndani ya dakika 20 kipindi cha kwanza kwa lengo la kuwaondoa mchezoni wapinzani wao hao.


 


Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. Katika kuelekea mchezo huo, Jumatano usiku kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar kikitokea Mwanza kucheza na Gwambina na moja kwa moja kikaingia kambini kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni, Dar.


 


Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze alisema kuwa anazipenda mechi za dabi hivyo hana hofu, kikubwa ameandaa mipango mikakati kwa wachezaji ili kuhakikisha anapata ushindi wa mapema katika mchezo huo.


 


“Malengo yangu ni kuimaliza dabi kwa kupata ushindi wa mapema na kufunga dakika za mwanzo hadi kufi kia 20, hilo linawezekana kwetu, kwani maandalizi niliyoyafanya yanatosha kupata ushindi. Siyo mchezo mwepesi kwani wapinzani wetu nao wamejiandaa vizuri, lakini kama kocha nimepanga kuingia kitofauti katika mchezo huo.


 


“Mchezo huo unahitaji mbinu, akili na ufundi mwingi ili kuwazidi wapinzani wetu, kikubwa niahidi kucheza mchezo mzuri wa kuvutia kwani uwanja tutakaoutumia ni mzuri tofauti na ule tuliocheza dhidi ya Gwambina,” alisema Kaze na kuongeza.

Post a Comment

0 Comments