Kaze: Yanga Ninayo Itaka Hii HapaWAKATI akikaribia kutimiza siku 30 tangu akabadhiwe mikoba ya kuifundisha Yanga, kocha wa kikosi hicho, Cedric Kaze amefunguka kuwa kuna mwanga ambao anauona wa timu hiyo kwenda anapopataka.


 


Kocha huyo ameongeza kwamba, hilo linatokana na wachezaji wake kuongezeka viwango pamoja na hali ya upambanaji wa timu yake kwa jumla. Kaze alitua nchini Oktoba 15, mwaka huu na kuanza kuinoa Yanga akichukua mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa.


 


 “Baada ya kukaa na timu kwa zaidi ya siku 22, naanza kuona tunaimarika lakini tuna nafasi ya kujiimarisha zaidi kwa mchezaji mmojammoja na timu pia.


 


 “Kuna hali ya upambanaji ambayo ipo kwetu kwenye kila mchezo ambao tunaingia uwanjani ambayo inaongezeka kila baada ya mechi moja, hali hii najua itatusaidia sana kwenye kupata matokeo mazuri kwenye mechi.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE