11/06/2020

Kenyatta: Tumechangua Maambukuzi ya Corona Kuongezeka KenyaKATIKA hotuba yake kwa Taifa la Kenya, Rais Uhuru Kenyatta amekubali kuwa mikutano ya kisiasa iliyoshamiri katika mwezi uliopita ilichangia ueneaji wa Virusi hivyo.


 

Mwezi Oktoba, viongozi wengi walifanya mikutano ya hadhara katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo bila kujali raia waliokuwa wakiwahutubia walikuwa wakigusana na wengi hawakuvaa barakoa.


 


Kenyatta amesema, “Ninawaomba Viongozi tuongoze kwa kuwa mstari wa mbele. Tusiwe wa kusema na kutenda tofauti. Ni jukumu letu kusema na kutenda yale ambayo tunawaambia wananchi wafuate.”


 


Katika mwezi wa Oktoba, maambukizi ya Virusi hivyo yalifikia 15,000 na vifo takriban 300. Wataalamu wa Afya wanaamini hii ilichangiwa na jinsi baadhi ya kanuni za kupambana na Corona Virus zilivyolegezwa.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a comment

Loading...

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger