11/02/2020

Kiduku: Nimetimiza Ahadi YanguBONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini anayepigana kwenye uzito wa Super Welter, Twaha Kassim ‘Kiduku’ amesema anashukuru kwa kuweza kutimiza ahadi yake ya kumchapa kwa TKO bondia Mthailand, Sirimongkhon Singwancha Lamthuam usiku wa Ijumaa.


Kiduku aliibuka mshindi kwenye pambano hilo lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, baada ya Mthailand huyo kusalimu amri kwenye raundi ya saba ya pambano kufuatia mashambulizi makali ya Kiduku.


Akizungumza na Championi Jumatatu, baada ya kuibuka na ushindi kwenye pambano hilo, Kiduku alisema: “Niliwaahidi mashabiki wangu kuwa yule Mthailand atakaa mapema, na asingemaliza pambano kutokana na ngumi kali ambazo nilikuwa nimemuandalia.


“Nashukuru kwa sababu nimetimiza ahadi yangu lakini pia nafurahi kwa sababu nimeliwakilisha taifa langu vizuri na sijawaangusha Watanzania wote waliokuja kunisapoti.”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger