Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kikosi cha PSG chakwama ndani ya lifti UjerumaniWachezaji 11 wa kikosi cha PSG walikwama kwa zaidi ya dakika 50 ndani ya lifti wakati wakitoka kwenye hoteli waliyofikia nchini Ujerumani wakielekea katika maandalizi yao ya mchezo wa Champions League dhidi ya wenyeji RB Leipzig.

Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne wakati nyota 11 wa PSG wakitoka kwenye hoteli waliyofikia wakielekea katika maandalizi ya mechi hiyo iliyopigwa usiku wa Jumatano na kushuhudia Paris Saint-Germain Football Club ikipigwa kwa jumla ya magoli 2 – 1 dhidi ya wenyeji RB Leipzig.


Kwa mujibu wa Le Parisien, kundi kubwa la wachezaji walikwama katika lifti zaidi ya dakika 50 na kuokolewa na ‘firefighters’.  Beki wa PSG, Layvin Kurzawa aliposti klip katika Instagram inayowaonesha ‘firefighters’ wakijaribu kuwanasua.


Angel Di Maria and team-mate Kurzawa were two of the PSG stars who were stuck in the lift


Hata hivyo baadaye alifutiliambali kipande hiko cha video licha ya kuwa ameshachelewa kwa kuwa mashabiki wengi walikuwa wameshaanza kutumiana kupitia mitandao ya kijamii.


PSG and Leipzig both trail Manchester United in Group H of the Champions League


Taarifa kutoka Ufaransa zinadai, Kurzawa alikwama na wenzake Presnel Kimpembe, Leandro Paredes, Angel Di Maria, Marquinhos, Bandiougou Fadiga, Abdou Diallo, Idrissa Gueye, Moise Kean, Colin Dagba na Kays Ruiz-Atil.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments