11/09/2020

Kimenuka huko, Young Dee chupuchupu kwa Chidi Benz

 


Wikiendi iliyopita msanii Young Dee alizindua 'EP' yake ya Dar Es Salaama  ambayo aliweza kuwaalika mastaa kadhaa kama Billnass Belle 9 Nyandu Tozzy Uchebe na wengineo ili kumsindikiza, kutoa sapoti na kufanya show kwa pamoja.

 

Show ilienda vizuri, watu wengi walitokea ili kushudia kitu ambacho amekifanya Young Dee ila wakati inamalizika kulitokea sintofahamu kati ya Chidi Benz na Younge Dee ambapo Chidi alitaka kulipwa na msanii huyo baada ya kutokea kwenye tukio hilo.


Akifafanua zaidi tukio hilo Young Dee ameeleza kuwa  "Chidi Benz naye alikuwa na akili zake za usiku siwezi ku-complain, sio surprise kwa Chidi kuwa na moment kama ile hakuna kitu chochote kilichoharibika, sidhani kama nina matatizo na chidi na kilichotokea sidhani kama kitaleta tofauti kati yetu,  kikubwa ni kutoelewana nikijaribu kumuelewesha hataki kunisikiliza lakini lugha ilikuwa gongana".


Pia Young Dee amesema anaamini ipo siku Chide Benz atamuelewa kuhusu tukio hilo baada ya kutofautiana na kushindwa kufikia makubaliano na maelewano kwa njia ya maneno.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger