11/02/2020

Kimenuka...Mbowe, Wenzake Mbaroni Tuhuma Kupanga MaandamanoKAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kupanga maandamano.


Viongozi wa Chadema wanaowashikilia ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless Lema, Isaya Mwita (aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam) na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa

wamepanga kuanza maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo kuanzia Novemba 2, mwaka huu kwa kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta

Aidha, jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo polisi wamesema ni ya vurugu kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa chama cha ACT Wazalendo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

2 comments:

 1. Na Kigulu pia mwenye ulimi mchafu
  mkosa adabu na maadili akiwemo mwenye
  chama mfukoni katika Flashi.

  Ndugu wana Habari nyinyi mna mchango
  mkubwa katika kuhabarisha umma Umuhimu
  wa Amani na hasara za kuhamasika katika uvunjifu wake.

  Wana Usalama msiwaonee muhali wala huruma ni zao ni ovu tena ovu sana.

  tafuta Mzito na Nonda na Sheibu wenzao
  walikuwakatika hatua za mwisho katika
  mlolongo wa vilipukaji na kundi la zitwo kule visiwani.

  Hawa wanataka muamalawa mkono wa chuma

  Endeleeni na Hongereni wana Ulinzi na
  Usalama na Pongezi kwa watoa habari za
  hawa mahaini wa taifa.

  ReplyDelete
 2. Na Kigulu pia mwenye ulimi mchafu
  mkosa adabu na maadili akiwemo mwenye
  chama mfukoni katika Flashi.

  Ndugu wana Habari nyinyi mna mchango
  mkubwa katika kuhabarisha umma Umuhimu
  wa Amani na hasara za kuhamasika katika uvunjifu wake.

  Wana Usalama msiwaonee muhali wala huruma ni zao ni ovu tena ovu sana.

  tafuta Mzito na Nonda na Sheibu wenzao
  walikuwakatika hatua za mwisho katika
  mlolongo wa vilipukaji na kundi la zitwo kule visiwani.

  Hawa wanataka muamalawa mkono wa chuma

  Endeleeni na Hongereni wana Ulinzi na
  Usalama na Pongezi kwa watoa habari za
  hawa mahaini wa taifa.

  Amani yetu ni Jukumu la Kila Mtanzania

  ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger