Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Kiongozi Yanga juu ya kuihujumu klabu yake

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMkurugenzi wa Sheria na wanachama wa Yanga,Patrick Simon mchana wa hii leo ametoa waraka kukanusha tuhuma anazopewa na baadhi ya watu kuwa anaihujumu timukwa watani wao Simba.

Waraka huo wa Patrick Simon ambaye pia ni kaibu katibu mkuu wa Yanga umefafanua mambo matano ambayo baadhi ya watu na moja ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo alitamka hadharani kuwa anawahujumu kwa mahasimu wao klabu ya wekundu wa msimbazi Simba.


Kupitia mitandao yake ya kijamii, Patrick Simon ameanza kwa kujibia tuhuma anayoshushiwa kuwa anakutana kkwa siri na baadhi ya viongozi wa wapinzani wao Simba ikiaminika kuwapa taarifa za nyeti za klabu ya Yanga kwa Wapinzani wao ameandika kuwa.

“Nakiri kukutana na mtendaji mwenye cheo kama changu kama alivyomtaja maeneo ya Yatch Club lakini sio vikao vya siri kwani kilichonikutanisha na mtendaji huyo ni swala la muhimu ambalo viongozi wangu wakubwa watatu walikuwa wanajuwa na walinipa baraka zote, na mara baada ya kikao hicho nilirudisha mrejesho wa kilichonipeleka. Na hii tunaongelea tarehe 20/10/2020 hivyo hakuna siri yeyote ”.

Hilo likiwa mosi, pili ni kuhusu tuhuma ya kufanyakazi kwa kuihujumu Yanga kwasababu anahofu ya kupoteza nafasi ya ukaimu katibu mkuu kwa aliyekuwa afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba msimu uliopita Senzo Mazingisa ili kuandaa mazingira ya kupokelewa Simba endapo akiondoka Yanga.

Patrick ameandika“Mimi nakaimu nafasi ya katibu mkuu lakini nimeajiriwa kama mkurugenzi wa sheria, hivyo basi siwezi kumhofia Mr.Senzo kwani yeye sio mwanasheria bali ni mshauri wa klabu”.

Tuhuma inayomuumiza Patrick ni kuambiwa aliihujumu kesi ya Bernard Morisson kwa Simba.


Kiongozi huyo alifafanua ya kuwa “Mimi ndiye niliyetengeneza ule mkataba kwahiyo kisheria nilikuwa sifudhu kutetea ile kesi, hivyo basi klabu iliamua kuweka wabobezi wawili ambao wamenizidi seniority kuweza kupambana na hiyo kesi na ndiyo wamaotuwakilisha huko CAS”.


Masikio ya wapenzi wa Yanga na wafuatiliaji wa soka nchini yamesubiri kwa muda kusikia hatma ya kesi ya Yanga kwenye mahakama ya usuluhishi ya masuala ya kimichezo Duniani CAS juu ya uhalali wa mkataba wa mchezaji Bernard Morisson ambaye hivi sasa anakipiga kwa watani wao wajadi.


Katika waraka wa kujibia tuhuma zinazomkabiri, Kaimu khatibu mkuu wa Yanga Patrick Simon amegusia kesi hiyo.

“Kesi yetu CAS imesajiliwa kwa namba CAS2020/A/7397. Hii maana yake ni kesi ya 7397. Ikumbukwe CAS inapokea kesi kutoka nchi ambazo ni wanachama wa FIFA dunia nzima, na ina kesi nyingi sana kama ilivyo mahakama ya rufaa ya Tanzania. Hivyo msiwe na haraka sana kwenye masuala ya sheria”. Alimalizia hivyo Patrick.

Vilevile Shauku ya wapenzi wa yanga na wafuatiliaji wa soka nchini ilikuwa ni kutaka kujua ni kesi ngapi ambazo yanga wamezipeleka kwenye shirikisho la soka nchini na zimefikia wapi, kaimu katibu huyo amefafanua kwenye waraka wake maana ametuhumiwa kutokuzipigania kesi hizo kwa kulinda maslahi ya Simba.

“Mpaka sasa Yanga ina kesi nne ambazo Shirikisho limeamua kuzipotezea, kesi ya kabwili, Morisson kuhongwa $5,000 kushawishiwa kuihama Yanga, Pingamizi la usajili wa Morrison na kesi ya mkataba wa nyota huyo wa Ghana ambao haujasainiwa na pande zote mbili na nina ushahidi wa kujitosheleza kwamba hizi kesi bado ziko pending kwenye shirikisho letu tukufu”.

Tuhuma ya Mwisho ni Kiongozi huyo kutopokea simu za mwenyekiti wa klabu hiyo na baadhi ya viongozi, “Hili suala sitolitolea maelezo kwani mwenyekiti ndiye mtu ninayeongoza kwa kuwasiliana nae katika viongozi pale klabu”. Patrick akasisitiza.

Mwisho akamaliza kwa kuandika “Kwa nafasi yangu kama ningekuwa mtu wa kuihujumu klabu ningekuwa Milionea mpaka sasa, mimi nimekula kiapo cha maadili ya kazi yangu, mpaka natoka yanga siwezi kufanya jambo lolote la kuihujumu klabu ambayo kwangu ni kama dini. Muda utaongea, Muda ni wetu sote. Daima mbele nyuma mwiko”.

Post a Comment

0 Comments