Kipigo cha Yanga Chamfukuzisha Kazi kocha wa Azam

ARISTICA Cioaba amefutwa jumlajumla kazi ndani ya Azam FC msimu wa 2020/21 kutokana na matokeo mabaya aliyopata hivi karibuni.

 

Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari Zakaria Thabit umesema kuwa mchakato umefanyika kuanzia timu ilipopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi zilizofuata timu ilicheza chini ya kiwango.

 

“Timu imekuwa ikicheza chini ya kiwango baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar, hata tuliposhinda mbele ya Dodoma Jiji bado hakukuwa na kiwango bora.

 

“Kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Yanga hali ilikuwa hivyo na tumepoteza hivyo makubaliano ya pande zote mbili tumefika makubaliano na kwa sasa Vivier Bahati atakuwa Kaimu Kocha Mkuu,” amesema.

 

Cioaba amesimamia Kwenye mechi 12 amepata ushindi mechi 8 sare moja kichapo 3. Vipigo viwili mfululizo ilikuwa mbele ya KMC na Yanga kwa kufungwa bao mojamoja. Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 18 na ile ya ulinzi imefungwa mabao sita.

 

🔴 TAARIFA 🔴

Azam FC tunapenda kuwataarifu mashabiki wetu na familia ya wapenda soka kwa ujumla kuwa tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu Aristica Cioaba, juu ya kusitisha mkataba wake.

Makubaliano haya pia yanamhusu Kocha wa viungo, Costel Birsan, wote wakiwa raia wa Romania. Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Bahati Vivier, kutoka Burundi, hadi pale tutakapotoa taarifa nyingine.

Tunawashukuru Cioaba na Costel, kwa mchango wao chanya walioutoa kwa kipindi chote walichohudumu ndani ya timu hii na tunapenda kuwatakia kila la kheri popote watakapokwenda.

Cioaba ameingoza Azam FC kwenye mechi 50 za mashindano (Ligi Kuu na Kombe la FA), akishinda mechi 28, sare 11 na kupoteza 11.

“All The Best”


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments