11/17/2020

Kusah Aweka Wazi Kuwa Ndio Mwandishi wa Ngoma mpya ya Nandy na Ali Kiba


Nyota mpya wa muziki wa kizazi kipya, @_kusah_ ambaye pia anafahamika kama mtunzi na mwandishi wa nyimbo hapa nchini, ameweka wazi kuwa ndio mwandishi wa ngoma mpya ya Msanii @officialnandy akiwa na @officialalikiba iitwayo "Nibakishie"


#Kusah ambaye alipata ajali ya gari hivi karibuni, iliyopelekea kuumia kwa Mguu wake wa kulia, naye anakazi yake mpya iitwayo "Nilinde", yenye maudhui ya kumshukuru Mungu kutokana na matatizo aliyopata. Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram jioni hii, #Kusah ameandika, "👸 @officialnandy #NIBAKISHIE 🕊 Written by Me 🤴 link on her bio 🌍."

-

Wimbo huo uliotoka mwishoni mwa wikiendi, hakika ni mafanikio makubwa kwa #Nandy kwani anaweza kuwa ndiye msanii wa kike anayezidi kufanya vizuri kwa nyimbo za ushirikiano.


Ndani ya mwaka huu #Nandy ametoa nyimbo kadhaa zikiwemo Na Nusu, Acha Lizame akiwa amemshirikisha #Harmonize. Dozi, Do Me akiwa amemshirikisha #Billnas na zote zimefanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger