11/21/2020

Lamine Ashusha Presha Yanga, Arejea Uwanjani
BAADA ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki moja na nusu, nahodha na beki wa kati tegemeo wa Yanga, Mghana, Lamine Moro anatarajiwa kuwepo kwenye sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Namungo FC.

 

Mghana huyo alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha ya goti aliyoyapata wakati timu hiyo ilipocheza dhidi ya Simba Novemba 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

 

Yanga yenye pointi 24, Jumapili hii itavaana na Namungo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa 1:00 usiku.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa beki huyo amepona majeraha yake na yupo fi ti kucheza mchezo huo dhidi ya Namungo. Saleh alisema beki huyo alianza mazoezi ya pamoja na wenzake tangu wiki iliyopita baada ya Daktari Mkuu, Shecky Ngazija kumfanyia vipimo na kuthibitisha kupona majeraha hayo.

 

“Habari njema kwa mashabiki wa Yanga kuwa beki wao kipenzi Lamine amepona majeraha yake, hivyo anatarajiwa kuwepo katika sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Namungo.

 

“Kurejea kwake kutaimarisha safu yetu ya ulinzi inayoongozwa na yeye kama nahodha, kurejea kwa Lamine kumempa unafuu kocha Cedric Kaze katika kupanga kikosi kitakachokuwa bora na imara. “Maandalizi ya timu yanaendelea vizuri katika kuelekea mchezo wetu dhidi ya Namungo kabla ya kukutana na Azam FC, kikubwa tunahitaji ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ya ubingwa wa ligi,” alisema Saleh.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 [disqus]:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger