Lil Ommy amekuwa Mtangazaji wa kwanza Tanzania kupewa nafasi AppleMtangazaji wa Wasafi media (@lilommy ) amekua mtangazaji wa Kwanza Kutoka Tanzania kutengenezewa Playlist yake katika Mtandao huo , ukiachana na @rayvanny , @navykenzoofficial ambao walitokea katika Covers za Playlist ya AFRICA NOW !

Ikiwa tunaelekea kwenye Msimu wa Sikukuu (Holiday season) , Lilommy  amepata nafasi ya kutaja  Playlist yake ya Ngoma kali Kwa ajili ya Msimu wa Sikukuu katika Mtandao mkubwa wa kuuza Nyimbo Duniani @applemusic .


Swipe kushoto kuweza kuona baadhi ya Ngoma zinazopatikana katika Playlist ya @lilommy , Kupitia Instagram yake Tambwe ameandikaa ujumbe huu:-


“Kipindi cha Sikukuu kinakaribia ikabidi Apple Music wanicheki kutengeneza list ya ngoma kali ambazo watu wataruka nazo kipindi chote cha sikukuu, hii ndo list ya ngoma zangu kali nilizoshusha, Dunia itafurahia sound ya Bongo Fleva na Ngoma za Afrika kwenye list hii! Asante sana Apple Music kwa nafasi hii šŸ™ kwani kuna watangazaji wengi sana Afrika lakini kunicheki direct na kunipa shavu hili kwangu ni kitu kikubwa sana šŸ™ #HolidaySounds #AppleMusic #LilOmmy #THEMVP šŸ‘‘ Tag Wasanii unaowaona kwenye list hii šŸ“

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE